Jana wakati timu zao zikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi za leo za Kundi A za michuano ya Kagame Cup, makocha wa timu ya Gor Mahia ya Kenya na Khartoum National Club ya Sudan walikutana na kupiga stori kwa dakika kadhaa huku wakionekana kucheka na kufurahi.
Kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na Frank Nuttal wa Gor Mahia, timu zao zilikutana juzi kwenye uwanja wa Taifa na kutoka sare ya kufungana goli 1-1. Timu hizo tayari zimeshakata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo zote zikiwa na pointi saba lakini mpaka sasa Khartoum wakiongoza kundi A kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa mbele ya Gor Mahia.
0 comments:
Post a Comment