Lagos, Nigeria.
Mlinzi wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Supper Eagles,
hivi karibuni alitoa ushuhuda wa ajabu na kuwashtua watu wengi.
Taribo West ambaye alikuwa ni kivutio sana uwanjani enzi za ujana wake
akiwa na Supper Eagles sasa ameokoka na kuwa mchungaji.
Taribo alishuhudia kwamba alikuwa akipelekwa na meneja wake nchini
Senegal kwa waganga wa kienyeji ili aupige mwingi uwanjani.
Taribo West anasema alikatwa baadhi ya sehemu za ulimi, vidole na kisha
kupikwa jikoni pamoja na mambo mengine ili acheze vizuri akiwa uwanjani.
Beki huyo wa zamani wa kutumainiwa wa Nigeria ambaye amekuwa 'Pastor'
hivi sasa anasema alitembelewa na mwanamke wa Mungu, ajulikanaye kama sister
Ikemefunwa akiwa nchini Italia, na kisha kumuombea na kuutoa uchawi wote na kumuweka
mtu safi.
Baada ya kumaliza soka, Taribo West sasa anamtumikia Mungu kwa
kutangaza maneno yake.
0 comments:
Post a Comment