Jana usiku mechi ya kuwania kufuzu Europa League baina ya timu ya Kukesi na Legia Warsaw iliyopigwa nchini Albania ilivunjika.
Legia walioshinda 2-1 katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu ya kufuzu walijikuta katika wakati mgumu baada ya mchezaji wao, Ondrej Duda kupigwa na jiwe lililorushwa kutoka kwa mashabiki wa Kukesi.
Mchezo ulisimama wakati Duda akitolewa nje ya uwanja kwa machela akienda kupatiwa matibabu.

Mwanandinga huyo alifungwa plasta kichwani, akavua jezi yake iliyochafuka kwa damu na kurudi uwanjani, lakini mechi haikuweza kuendelea.

Polisi wakipambana na mashabiki huko Tirana

Jiwe lilitoka kwa mashabiki hawa wa Kukesi
Mpaka sasa Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA halijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment