Na Ramadhani ngoda.
Baada ya kumbwaga
Mphilopino Many Pacquiao, bondia ambaye hajaonja ladha ya kipigo katika mchezo
wa masumbwi, Floyd Mayweather Jr amethibitisha kupanda tena ulingoni Septemba
12 mwaka huu katika pambano linalotaraji kufanyika mjini Las Vegas Marekani.
Mayweather ambaye
ameshinda mapambano 48 aliopanda ulingoni bila sare wala kupoteza akishinda
mapambano 26 kwa ‘knockout’, anashikilia mataji ya WBC na WBA katika uzito wa ‘welter’
alidhihirishia ulimwengu ubora wake kwa kumtwanga kwa wingi wa alama mpinzani
wake Many Pacquiao katika pambao lilivunja rekodi ya mapato katika mchezo wa
ngumi ulimwenguni.
Mmarekani huyo
aliyepokonywa mkanda wa WBO baada ya kukiuka masharti mapema wiki hii, ametuma
ujumbe kwenye mtandao wa kijamii ukiashiria kurudi kwake ulingoni kabla ya
kuisha kwa mwaka huu.
“Kwa mashabiki wangu.
Uaminifu wenu na sapoti yenu vimenipa miaka 20 bora ambayo ningeiomba. Na
nikiwa juu, napanga kwenda juu. Tukutane tena ulingoni Septemba 12,” ulisomeka
ujumbe wa Mayweather.
Taarifa hizo zinaweza
kuibua fununu nyingi juu ya nani atavaana na bondia huyo katika pambano hilo
kwani mabondia kadhaa wameshatajwa kupanda naye ulingoni akiwemo Andre Berto
aliyeshinda mapambano 30 na 23 kwa ‘knockout’ pamoja na Karim Mayfield
aliyeshinda mapambano 19 huku 11 kati ya
hayo akimaliza kwa ‘knockout.’
Mwingine
anayevumishwa kupanda ulingoni na bingwa huyo ni bingwa wa zamani wa dunia Amir
Khan ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akisaka nafasi ya kuzichapa na
Mayweather bila mafanikio lakini itawabidi wapenzi wa ndondi kusubiri mpaka
itakapotangzwa rasmi ni bondia gani atakwenda kuendeleza au kuvunja rekodi ya
nguli huyo wa mchezo wa masumbwi ulimwenguni kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment