Bondia
asiyepigika, Floyd Mayweather amevuliwa mkanda wa ubingwa wa WBO, uzito wa
Welterweight unaohusisha kilo 67 na 77 ambao
alishinda mwezi Mei mwaka huu dhidi ya Manny Pacquiao kutokana na kushindwa kufuata sheria na kanuni za Shirikisho
hilo.
Kamati ya
mashindano ya WBO imesema kwamba haina jinsi ya kufanya zaidi ya kumvua mkanda
huo Mayweather ambaye ameshindwa kulipa ada kutoka kwenye pambano alilopigana
na Pacquiao.
Ijumaa
iliyopita, ilikuwa siku ya mwisho kwa Mayweather
kutimiza vigezo vya ubingwa wa WBO ikiwemo kulipa ada ya dola laki mbili kutoka
katika pambano lake na Pacquiao pamoja
na kujivua ubingwa wa uzito wa light-middleweight wa WBC na WBA.
Mayweather anayetajwa
kuwa mwanamichezo tajiri zaidi Duniani ameshindwa kutelekeza agizo hilo, hivyo kamati
imeamua kumvua mkanda wake wa kwanza wa
WBO.
Bondia Timoth
Bradley Jr anatarajiwa kupewa mkanda huo baada ya mwezi uliopita kumpiga
kiutata, Jessie Vargas katika pambano la kutafuta bingwa wa muda wa
uzito huo, ingawa Mayweather mwenye umri wa miaka 38 amepewa siku 14 za kukata
rufaa.
Mayweather bado anashikilia ubingwa wa welterweight na super-welterweight
wa WBC na WBA, ingawa
kisheria, bondia haruhisiwi kushika
ubingwa wa dunia kwa madaraja mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment