Matajiri wa Ufaransa, PSG mapema leo wametangaza kukamilisha usajili wa Benjamin Stambouli kutokea klabu ya Tottenham.
Mabingwa hao wa kandanda wa ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1 wamesema kiungo huyo mwenye miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano.
Huu ni usajili wa pili wa PSG majira haya ya kiangazi kwani tayari wameshainasa saini ya Golikipa wa Eintracht Frankfurt, Kevin Trapp.
Stambouli anaonekana kuwa mrithi wa Yohan Cabaye ambaye amejiunga na Crystal Palace mapema majira ya kiangazi.
PSG wameripotiwa kulipa paundi milioni 6 kumsajili kiungo huyo.
0 comments:
Post a Comment