Real Madrid wamerejea Hispania baada ya ziara ya mafanikio ya kujiandaa na msimu mpya huko Australia na China.
Kufuatia kuwachapa AC Milan kwa penalti 10-9 mjini Shanghai, China na kutwaa ubingwa wa International Champions Cup, jana usiku, Cristiano Ronaldo na wenzake walionekana kuwa na furaha baada ya kukanyaga ardhi ya nyumbani.
Mreno huyo alikuwa na tabasamu kwenye ndege sambamba na Pepe na Marcelo kabla ya ku-post picha akiwa anakula nyumbani kwake na kuandika maneno haya:
"Nilikimisi chakula cha nyumbani!!"
0 comments:
Post a Comment