Roberto Mancini amekiri kwamba alikuwa akimuonea wivu Jose Mourinho kushinda makombe matatu wakati alipokuwa akiifundisha Inter na kuongeza kuwa amefanya maamuzi ya kipuuzi kurudi kuifundisha klabu hiyo kwa mara nyingine tena.
Licha ya kushinda kombe la ligi kuu nchini humo mara tatu mfululizo katika kipindi chake cha mwanzo, Muitaliano huyo alifukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho katika msimu wa majira ya joto wa mwaka 2008.
“Sikutarajia kufukuzwa”, Mancini aliiambia Gazzetta TV.
“Nilisoma habari kutoka katika gazeti moja asubuhi ya siku hiyo, na wasiwasi fulani hivi ukanijia. Massimo Moratti aliniita na kuniambia kwamba yale ndio maamuzi aliyochukua.
“Alimtaja Mourinho? Hapana. Sio mbaya acha tu nimshukuru Moratti, kwa sabbabu alinipa fursa ya kuwa kocha wa Inter kwenye wakati ambao ulikuwa ni muhimu sana katika maisha yangu”.
Alipoulizwa kuhusu Mourinho, Mancini alijibu: “Nadhani ni kocha mzuri. Je nina wivu juu ya makombe matatu? Hizi ni fikra zilizopo ndani, lakini naamini vitu hivi vilitokea kwa sababu vilipangwa kutokea”.
0 comments:
Post a Comment