Monday, July 13, 2015

Manchester United imetangaza kikosi kinachoenda katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya 'pre-season tour party' nchini Marekani na Stori kubwa ni kuchaguliwa kwa golikipa wa mashetani hao wekundu, David De Gea.
Licha ya muendelezo wa tetesi za kutimka Old Trafford kwenda Real Madrid majira haya ya kiangazi, De Gea mwenye miaka 24 amejumuishwa kwenye kikosi hicho, huku Golikipa namba mbili wa United, Victor Valdes akiachwa kwenye orodha hiyo.
Kukosekana kwa Valdes kumewashangaza wengi na kuongeza tetesi kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Memphis Depay, Morgan Schneiderlin, Matteo Darmian na Bastian Schweinsteiger  wamejumuishwa pia.
Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi ni Angel Di Maria na Marcos Rojo (ambao wote walicheza Copa America). Pia mlinzi wa kulia Rafael ameachwa.
Man United wanakwenda kushiriki kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambapo Kikosi hicho  cha Van Gaal kitacheza mechi nne Marekaini dhidi ya Club America, MLS side San Jose Earthquakes na miamba ya Ulaya Barcelona na PSG.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video