Klabu ya Mnchester United inakaribia kukamilisha dili la kumsajili beki wa kulia Matteo Darmian baada ya majadiliano kati ya United na klabu ya Torino ya Italia kufikia hatua nzuri.
United wanahitaji mchezaji ambaye anaweza kucheza kama mlinzi wa kulia baada ya kocha wa kikosi hicho Louis van Gaal kusema kwamba, Mbrazil Rafael ameshindwa kuimudu nafasi hiyo.
Ieleweke kwamba, Man United imekuwa kwenye mazungumzo na Darmian, 25, na wana matumaini ya kufikia makubaliano ya kumsajili nyota huyo kwa kiasi cha pauni milioni 11.
Darmian ni mchezaji wa kimataifa wa Italia ambaye ameshaitumikia timu yake ya taifa kwa michezo 13 na michezo sita akicheza muda wote (full time), Van Gaal anaamini mchezaji huyo atamsaidia kwenye nafasi ya ulinzi wa kulia.
Pia Van Gaal anatarajia kumuachia Rafael aondoke kabla ya kuanza kwa msimu mpya lakini atasikiliza ofa pia juu ya mlinzi wa kati John Evans ambaye mpaka sasa bado hajapewa mkataba mpya.
0 comments:
Post a Comment