Mama wa Iker Casillas ameamua kuomba radhi kwa kauli yake ya kwamba mwanaye anapaswa kuchezea timu bora zaidi ya Porto.
Kwa pamoja, Mari Carmen Fernandez na mumewe, Jose Luis, walibaki na msimamo wao kwamba mtoto wao alikuwa hapati heshima anayostahili katika klabu yake ya Real Madrid, ambayo Jumamosi aliaga rasmi kutimka klabuni hapo kuelekea maskani yake mpya katika klabiu ya Porto.
Mama wa Casillas alienda mbali zaidi kwa kuwafananisha wababe hao wa Dragao katika timu za daraja la tatu lakini ameamua kuomba radhi kwa tukio hilo.
"Pengine sikuwa sahihi", alikaririwa na gazeti la Marca.
"Nataka kuwashukuru Porto kwa kumsajili mwanangu. Natumaini watafanya kazi bega kwa bega ili kuipa mafanikio klabu. Ningependa mnisamehe mara 1,000. Natumaini mwanangu atapata mafanikio kama alivyopata akiwa Madrid.
"Iker alifanya majaribio yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 8. Mara zote alikuwa akijitoa asilimia zote kwa ajili ya klabu. Siku zote amekuwa ni mwenye nidhamu na heshima kubwa.
"Nadhani mashabiki wamekuwa ni watu wema sana kwa mwanangu. Nimekuwa nikishuhudia, kwa moyo mkunjufu mashabiki wakimshangilia mwanangu pindi atokapo uwanjani".
0 comments:
Post a Comment