Tuesday, July 14, 2015

Waziri wa Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi, Julai 18 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Magufuli baada ya kufungua rasmi michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukindoa mecho ya Yanga Vs Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al Shandy uwanja wa Taifa saa 8 mchana, KMKM Vs Telecom saa 10 jioni uwanja wa Karume.
Kuanzia leo tutakua tunawaleta kwa ufupi timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu, na kwa kuanza tunaanza na kundi A;
Mchezo wa ufunguzi  kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia unaonekana kuteka hisia za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani ni takribani miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika ardhi ya Tanzania.
Mara ya mwisho mwaka 1996 katika michuano ya Cecafa, timu hizo zilikuwa katika kundi moja, katika mchezo wa awali zilitoka sare ya bao 1- 1, wakati zilipokutana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Gor Mahia iliibuka na ushindi wa mabao 4 -0.
Gumzo la wadau wa soka nchini kwa sasa ni kuhusu uwezo wa klabu za Tanzania, Yanga, Azam na KMKM kuweza kuhakikisha kombe la michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki haliondoki kwenye ardhi ya
Tanzania.
Kwa upande wa Yanga, matumaini ya kulibakiza kombe kwenye ardhi ya Tanzania yatachagizwa na historia yao nzuri ya miaka ya hivi karibuni pindi Kombe la Kagame linapoandaliwa nchini. Yanga iliibuka kidedea mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012 mashindano hayo yalipoandaliwa nchini.
Yanga mabingwa mara tano wa michuano hio watakuwa na kazi moja tu ya kujaribu kuifikia rekodi ya Simba, inayoongoza kutwaa Kombe hilo mara nyingi, ikiwa imeweza kufanya hivyo, mara sita.
Kocha: Hans van Pluijm ( Uholanzi)
Yanga iko chini ya mtaalam kutoka Uholanzi, Hans van Pluijm anayesifika kwa kuwa mfuasi asiyetetereka  wa soka la kushambulia.
Nyota wa kutazamwa:
Yanga ina wachezaji kadhaa inaowategemea ili kufanya vizuri. Macho na masikio yataelekezwa kwa Donald Ngoma,  mshambuliaji aliyesainiwa kutoka Platinum Fc ya Zimbabwe kuona kama ataendeleza kasi yake ya ufungaji aliyoanza nayo.
Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Nadir Haroub na Amissi Tambwe ni kati ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuendelea kuwa nguzo za Yanga kwenye michuano hii.
Rekodi kwenye Kombe la Klabu Bingwa:
Yanga imebahatika kutwaa ubingwa mara tano; (Mwaka 1975, 1993, 1999, 2011, na 2012).
Pia Yanga imemaliza kama washindi wa pili mara mbili, mwaka 1976 ilipofungwa na Gor Mahia 2-1 jijini Kampala na mwaka 1992 ilipolala kwa mikwaju ya penati mbele ya watani wao wa jadi, Simba.
Kuanzishwa:
Yanga ilianzishwa mwaka 1935, na kuwa moja ya klabu kongwe kabisa kwenye ukanda huu na bara la Afrika kwa ujumla.
Gor Mahia: Wababe wa Kenya waliojipanga upya kurudisha heshima.
Gor Mahia hawakufanya vizuri katika michuano ya mwaka jana, ila wanatarajiwa kutoa ushindani katika mashindano ya mwaka huu.
Licha ya kupotea kwa muda mrefu kabla ya kuibuka na kushindwa kufurukuta kwenye michauno ya mwaka jana jijini Kigali, Gor Mahia wanajipa moyo Zaidi kutokana na mwenendo wao kwenye Ligi ya
Kenya.
Mabingwa hao wa Kenya hawajapoteza mechi msimu huu huku wakionesha dalili za kutangaza ubingwa mapema kabisa.
Kundi lake:
Gor Mahia iko kwenye kundi A la michuano ya mwaka huu ikijumuishwa na Yanga, Al Khartoum ya
Sudan, KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibout. Ni kundi ambalo ni gumzo kuu likdaiwa  kuwa na mechi zenye msisimko Zaidi na ushindani mkubwa.
Wachezaji wa kuangaliwa:
Kwa wafuatiliaji wa soka nchini Kenya, hakuna anayepinga kuwa kwa sasa timu yenye wachezaji bora zaidi ni Gor Mahia.
Wachezaji kama Khalid Aucho, chipukizi Micheal Olunga anayetajwa kuwa mrithi wa mshambuliaji bora kuwahi kutokea nchini Kenya, Dennis Oliech, na Meddie Kagere wamekuwa ni kiungo muhimu kwenye timu hii.
Wachezaji wengine ni pamoja na mlinda mlango Boniface Oluoch zake kutikiswa kwenye ligi ya Kenya inayoendelea kwa sasa.
Mlinzi wa Uganda Cranes, Godfrey Walusimbi na George Odhiambo wakiongeza chachu kwenye timu hiyo.
Benchi la Ufundi:
Gor Mahia inaongozwa na kocha Frank Nuttal, raia wa Uskochi. Benchi lao la ufundi linajumuisha pia mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Harambe Stars, Mathew Ottamax ambaye ana jukumu la kuwanoa walinda mlango, Boniface Oluoch na Jerim Onyango.
Rekodi Kombe la Kagame:
Mara ya mwisho Gor Mahia ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1985, lakini imetwaa ubingwa huo mara 5 (1976, 1977, 1980, 1981, 1985).
Wakati huo huo kuelekea kuanza kwa michuano ya Kagame siku ya jumamosi, waamuzi wa michezo hiyo wanatarajiwa kuwasili kesho siku ya jumatano sambamba na kamati ya ufundi kwa ajili ya mitihani ya utimamu wa mwili (Physical Test) siku ya alhamis, na kamati ya ufundi watakua wakikagua viwanja na kuweka vipimo kabla ya ufunguzi rasmi wa michuano hiyo siku ya jumamosi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video