MAAFISA wa FC Lupopo ya DR Congo wametua makao makuu ya
Yanga, mitaa ya Jangwani, Kariakoo, Dar es salaam kudai fedha za usajili wa
Mbutu Twite.
Mwaka jana, Yanga walikubaliana na Lupopo kumsajili Twite
kwa mkataba wa miaka miwili, lakini mabingwa hao wa Kandanda Tanzania bara
wakaamua kumsainisha mwaka mmoja.
Baada ya mkataba huo kumalizika, Yanga wamemuongeza mwaka
mwingine na Lupopo waliposikia Twite kaongeza
mwaka mwingine, wakajua Wanajangwani wameenda kinyume na makubaliano ya awali.
Wakafunga safari kuja
Dar es salaam na jana wamekutana na katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha wakidai
waongezwe hela za usajili wa Twite, lakini Daktari huyo wa michezo amewapa
maelezo ambayo wameonekana kuridhika.
Dr. Tiboroha amezungumza na mtandao huu na kuthibitisha kwamba viongozi wa Lupopo wamefika Ofsini kwake.
“Hii ishu ilitatuliwa toka mwaka jana, kwanza nikupongeze!, umeipataje
hii taarifa? Yanga mwaka jana walifikia makubaliano na FC Lupopo, ilifanya
mazungumzo na Rais wa FC Lupopo, Bwana Kasongo na kukubaliana Yanga itoe kiasi
ilichotoa (hajataja) ili iweze kumsajili Mbuyu Twite kwa miaka miwili”. Amesema
Tiboroha na kuongeza: “Mwaka jana Mbuyu Twite alitakiwa asaini kwa miaka
miwili, lakini Yanga baada ya kufanya makubaliano ilimsajili kwa mwaka mmoja”.
“Kilichowashangaza Lupopo mwaka huu ni kusikia Mbuyu Twite
ameongeza mkataba wa mwaka mwingine,wam ekuja kudai hela. Walipofika jana, mimi
nikaingia kwenye nyaraka na kuwaonesha vitu, kilichonishangaza pia ni kwamba
wanadai yale makubaliano hawakuyapata japokuwa walipokea hela bila kupata
mkataba wowote. Haya mambo tumeyaongea vizuri jana na wameonekana kuelewa”.
0 comments:
Post a Comment