Danny Ings
Danny Ings amepiga hat-trick dhidi ya Felda United ya Malaysia katika muendelezo wa mechi za maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza ambapo Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 7-0.
Japokuwa ni mchezo wa majaribio tu, lakini imekuwa ni fursa nzuri kwa Brendan Rodgers kumwona mshambulizi wake huyo huku akiangalia jinsi ya kumjumuisha na mshambulizi mpya aliyesajiliwa kutoka Aston Villa Christian Benteke.
Magoli mengine yamefungwa na Lazar Markovic Pedro Chiravella, Sheyi Ojo na Joao Carlos Teixeira.
KIKOSI CHA LIVERPOOL KILIKUWA:
Fulton, Wisdom, Toure, Sakho, Maguire, Ojo, Rossiter, Chirivella, Markovic, Teixeira, Ings
Divock Origi
0 comments:
Post a Comment