Real Madrid leo wameichapa 4-1 Manchester City nchini Australia katika mechi ya maandalizi ya msimu na kumaliza vinara kwenye msimamo wa mashindano ya International Champions Cup, yaliyojumuisha pia klabu ya AS Roma.
Baada ya mechi hiyo, Real Madrid walipata kombe ambapo Alvaro Arbelo na Cristiano Ronaldo walinyanyua ndoo hiyo.
Cha kushangaza, Sergio Ramos hakuwepo kwenye tukio hilo wakati yeye ndiye nahodha wa timu baada ya Iker Casillas kuondoka.
Ramos alitolewa na akamkabidhi kitambaa cha unahodha, Arbeloa, lakini bado Ronaldo alirudi kubeba kombe.
Ramos alikuwa wapi?
Hata kama ni kombe la Pre-season, ilifikirika kwamba ingekuwa bahati kwa Ramos kubeba kombe kwa mara ya kwanza akiwa nahodha.
Au alikuwa na majukumu mengine?
Kama kweli Ramos anataka kujiunga na Manchester United, majira haya ya kiangazi huenda hakutaka kunyanyua kombe hilo.
0 comments:
Post a Comment