Thursday, July 23, 2015


Nikiwa naangalia video za mitandaoni, ghafla niliona "video clips" moja hivi imeandikwa "Gustavo de ma limma" nikavutiwa na sura ya vijana wawili ambao walikuwa wamekusanya maelfu ya Wabrazili pale ukumbini, mmoja alikuwa anafanana na Suarez japokuwa yeye ni mwembamba sana, ila huyu mwingine ambaye amependeza zaidi ya mwenzake ana sura ya kike, tena leo amenyoa masharafa na ndevu zake, kwakweli anavutia sana, warembo wa ki Brazili wanaonekana kutaja jina lake pale
anaposhika kipaza sauti, ni ngumu kuamini kama anafahamu kucheza soka, ukimuangalia ni kama mlaini sana.... hatimaye namaliza kutazama....

Baada ya kutazama "video clip" hii nalazimika kumfatilia huyu "braza-men", kwanini anashangiliwa sana? ni sura yake inayovutia au? je, ana kipi kingine mbona hata pale kwenye stejini hakuwa na lolote? Anyway kwakuwa sikuwa na jibu nikampigia "My brother from another mother" nyie mnamuita "Fundi Shaffih Dauda" ila mimi namuitaga Braza
shaffi, baada ya kumuadithia nilichokiona akacheka sana akanambia huyo ni Mchezaji bora wa Dunia anaekwenda kuwashikia chini Messi na Cr7 siku zijazo...., nikapata mwanga kutoka kwa Braza Shaffi. Tuachane na
hayo em leo tutazame tuzo za Mchezaji bora wa Ulaya wa msimu....
Miongoni mwa waliotajwa yupo kijana mdogo sana anaepewa majukumu makubwa kwenye nchi yake pindi anapokwenda America, kuna vitu vimenigusa hadi nachukua kalamu na karatasi kuandika juu ya kinda huyu
ambae kwa ufupi wanamuita "Neymar Junior" kwa wale ambao hadi sasa hawajajua ni nani hasa namzungumzia..!! Sina haja ya kumuelezea alipotoka hadi hapa alipo, ila ninayo haja ya kuzungumzia "perfomance"
yake kwa msimu uliomalizika, hapana shaka utakubaliana na mimi kuwa huyu "Dogo" anastahili kuingia "Top 3" au hata kuchukua kabisa hii tuzo, naomba tuwe pamoja tafadhali..
Tunapozungumzia "World Class Striker" ni mshambuliaji ambaye anaweza kukupa magoli angalau 19 katika mechi 38, kama haukukimbiaga hesabu utakuwa unaelewa nini namaanisha, inamaana unapaswa kufunga japo goli
moja kwenye mechi mbili, hapo nimeacha mambo ya assist na vitu vingine, nazungumzia idadi ya mechi na magoli, Neymar akiwa miongoni kwenye ule "Utatu Utakatifu" wa Fc Barcelona hakuwa mshambuliaji wa moja kwa moja na wala hakuwa mshambuliaji muongo muongo kama Messi la
hasha.! huyu alikuwa anapenda kushambulia kutoka pembeni kabisa na kuingia ndani kwa kasi ya ajabu, sasa ole wako umguse..! utakoma..
Kwa upande wa Ulaya Neymar ameonekana kuwa na mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi, akiwa na Fc barcelona kafanikiwa kufunga magoli 39 kati ya mechi 51, vipi umegundua nini hapo? tena hapo sijazungumzia
"Assist" wala magoli aliyoifungia Brazili. Ndani ya magoli haya, 10 ni ya Uefa Champion League, 22 ni ya La liga, alafu 7 ni ya Copa del rey, nikisema Neymar ni miongoni mwa wachezaji watano Ulaya waliojaliwa kufunga kwa sasa nitakuwa mnafiki? japokuwa hauipendi Brazili na Fc
Barcelona huna budi kumeza ndimu na kumkubali kwa tabu kijana huyu ambaye ana rekodi mbovu ya utovu wa nidhamu uwanjani.

Japokuwa majuzi aliigharimu timu yake ya taifa na kufanikiwa kufunga goli moja tu katika michuano, bado rekodi hiyo chafu haimzuii Neymar kutwaa tuzo hii, mbali na yeye kufunga kumbuka alikuwa na mchango kati
ya yale magoli 122 yaliyofungwa na "Utatu mtakatifu" nazani unakumbuka viwango vyake kuanzia robo fainali ya Uefa hadi fainali, naamin Neymar alistahili kuchukua kiatu cha ufungaji bora wa Ulaya ila kilichomkwamisha ni roho nzuri aliyokuwa nayo uwanjani, unakumbuka
mechi ya marudiano na Bayen pale Ujerumani? alichenga mabeki wote na kubaki na Nuer ila alikumbuka rafiki yake Messi bado hajafunga....

Alichokifanya ni kumpa pasi Messi ila siku ile bahati haikuwa kwa Messi. Pia kwenye kombe la mfalme nazani unakumbuka mchango wa Neymar hasa pale walipokutana na Atletco de Madrid, msimu uliopita alitengeneza nafasi 93 kwa Messi na nafasi 57 kwa Suarez japokuwa
Messi na Suarez hawakufunga kwenye nafasi zote.. kwa ufupi huyo ndo Neymar na mafanikio yake japo kwa uchache katika msimu uliopita, nafahamu yapo mengi sana hasa ndani ya uwanja kwani jamaa pia ni fundi wa kupiga "tackle" hasa pale wapinzani wanapokuwa na mpira ili asaidie kukaba na kuendeleza mapambano kule mbele...

Japokuwa hakuna binadamu aliyekamilika, Neymar naye anaonekana hajakamilika hasa kwa upande wa nidhamu, huyu "Dogo" akifanyiwa madhambi anataka mwamuzi atoe kadi, endapo atapeta basi Neymar "hu-panic" na kutoa maneno ya kufoka kwa Mwamuzi na hapa ndipo
alipopata kadi nyingi za njano hasa zile 10 za msimu uliopita na kufanya kuwa mchezaji mwenye nidhamu mbovu mbali na wale mabeki wanne wa nyuma. Hapa msimu ujao anatakiwa awe makini sana, pia hata "rate"
ya kutoa pasi kwa wakati na kuwafikia walengwa imepungua msimu huu tofauti na msimu uliopita, pia hapa anapaswa kukaza sana.

Hatimaye namuona Neymar akiwa miongoni mwa "Top 3"  kati ya wale 10 waliotajwa, pia namuona Neymar akiwa mchezaji bora wa dunia tena zaidi ya mara 2 hapo baadae..! pia namuona Neymar akichukua "Pichichi" na
kuvunja utemi wa Cr7 na Messi muda mchache ujao, lakini pia namuona Neymar akifungiwa mechi kadhaa kutokana na utovu wa nidhamu ambao ni kawaida yake, kabla sijamaliza namuona Neymar akidumbukia kwenye dimbwi la kashfa kama zile za ndugu yake wa kule kule America
anayeitwa Gaucho, nazani utakuwa umeungana na mimi japo kwa mbaali kwamba Neymar anastahili kuwa miongoni mwa wachezaji watatu bora Ulaya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video