Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kwamba kocha wa Arsenal Arsene Wenger anahitaji kupewa kalukuleta linapkuja suala la kufananisha kati ya Arsenal na Chelsea.
Mwanzoni kabisa Wenger alisema "isingewezekana" kwa Arsenal kushinda taji la ligi kuu kwa miaka kadhaa iliyopita, kitu ambacho amekipinga.
Mourinho aliiwezesha Chelsea kutwaa taji la EPL msimu wa 2014-15 na kuelekea msimu mpya wa ligi, anasema kwamba, kauli ya Wenger imejaa uongo mtupu.
“Kama utajumuisha timu zilizotumia pesa nyingi kwa miaka mitatu au minne iliyopita, nadhani utakutana na mshamgao mkubwa ", aliwaambia waandishi.
“Chukua kalukuleta. Hicho ni moja ya vitu rahisi kabisa kufanya. Itasaidia kuondoa utata wote. Kama unataka kuwa mkweli, usiyeegemea upande wowote na mtendaji wa kweli, basi hilo litakuwa ni jambo rahisi kwa kocha au mwandishi kufanya.
“Wamenunua golikipa imara kabisa, na hiyo ni sehemu ambayo ni muhim sana katika timu.
“Kama unamuweka Ozil ukaongeza na Sanchez, halafu Chambers, Debuchy utakutana na mshangao mkubwa sana”.
0 comments:
Post a Comment