Tuesday, July 14, 2015

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa Manchester United wamefanya usajili wa wachezaji wawili wa kiwango cha juu ambao ni Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin.
Baada ya kuisaidia United kushika nafasi ya nne msimu uliopita, Louis van Gaal ameamua kuingia haraka sokoni kuhakikisha anaimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa kampeni mpya huku akiwa na sura mpya kikosini kwake, ambazo ni Memphis Depay kutoka PSV, Matteo Darmian kutoka Torino, Bastian Schweinsteiger kutoka Bayern na Morgan Schneiderlin kutoka Southampton.
“Tulifahamu kuwa wasingekuwa na furaha baada ya kumaliza nje ya nafasi tatu za juu na ndio maana tulijua wangelishughulikia hili suala”, alisema Wenger.
“Wamefanya usajili mzuri. Walimaliza msimu huku wakiwa na fikra za kulijenga upya eneo lao la kiungo, na wamefanya hivyo kwa kusajili wachezaji wawili muhimu ambao ni Schweinsteiger na Schneiderlin. Ni wachezaji wa viwango vya juu sana.
“Kuna mmoja ambaye ndio anakuja sasa katika ubora wake ambaye ni Schneiderlin, na mwingine ambaye ameshafanya makubwa katika tasnia hii. Ni suala la kuvutia sana kuona namna ambavyo wameamua kuchanganya damu.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video