Nahodha wa Chelsea John Terry amesema Manchester City wamelamba dume baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya nyota wa Liverpool Raheem Sterling kwa ada ya pauni milioni 49.
Japokuwa usajili wake ulizua hali ya sintofahamu klabuni kwake, lakini Terry amesema kuwa suala la Sterling kung'ang'ania kwenda klabu inayoshiriki ligi ya mabingwa liko wazi kabisa.
"Sterling alikuwa ni moja ya wachezaji bora sana ambao nilikutana nao msimu ulioisha. Alisababisha mambo mengi sana na nadhani anaenda kuwa mchezaji mkubwa sana kwa Man City", aliwaambia waandishi.
"Suala hapa sio hela, bali ni mchezaji gani mwingine wa Kiingereza ungeweza kwenda kumnunua? Kwa upande wangu alikuwa moja ya wachezaji bora kabisa wa ligi msimu uliopita".
"Yamkini kuna baaadhi ya vitu ambavyo hakuvimudu vyema katika suala la uhamisho huu lakini nadhani ni kijana mdogo ambaye angependa kucheza katika ngazi za juu za vilabu, hivyo sidhani kama ana kosa lolote, alipaswa kwenda tu na kufanya hivyo kwa klabu ya Manchester City kwa sababu Liverpool hawakufanya vyema msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment