BAADA ya Yanga kufanya usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, amesema sasa kikosi kimekamilika.
Yanga wanajiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame itakayoanza keshokutwa, ambao wanafungua dimba na Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA juzi, Pluijm alisema klabu hiyo imefanya usajili kwa umakini ili kuhakikisha msimu ujao wanakuwa na timu imara.
Pluijm alisema ana amani Haji Mwinyi na Josephat Zuttah waliosajiliwa na Yanga kama mabeki wa pembeni watakuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment