Wednesday, July 8, 2015

PluijmMabingwa wa Tanzania bara Yanga SC leo wanashuka uwanjani kuwakabili ‘wanamaji’ KMKM kutoka Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm amesema wachezaji wake wanapaswa kucheza kwa weledi wa hali ya juu kwani sasa wapo kwenye maandalizi ya kombe la Kagame na atakaefanya vizuri ndie atapata nafasi.
“Kwangu mimi hakuna mchezo wa kirafiki unaelewa? Kama ni mwenye kufuata ueledi utakuwa unataka kushinda na hicho ndicho nachokijua, ninachokitegemea ni kucheza kwa nidhamu na kujiandaa kwa michuano ya Kagame na nadhani kila mmoja anatakiwa kufanya jitihada na mwenye ubora ndiye atakaepata nafasi”, Pluijm amesisitiza.
Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, mcheo huo utaanza saa 10:00 jioni ili kutoa nafasi kwa watu waliofunga kuwahi kufuturu.
“Mechi itaanza saa 10 ili kuwafanya watu wawahi kufuturu kwasababu unapoanza mechi umechelewa na foleni zetu za hapa mjini watu watachelewa kwenda kufuturu”, amesema Tiboroha.
“Kuna mapendekezo yalikuwa yametolewa, tuanze mechi saa tisa lakini hatujafikia muafaka huo. Lakini mashabiki wetu na wengine wenye nia njema na Yanga na ambao si mashabiki lakini ni wanazi wa sehemu nyingine tunawakaribisha waje waone mziki wetu”, alimaliza.
Mchezo huo unalengo la kujipima nguvu kwa timu zote hizo ambazo zitashiriki michuano ya kombe la Kagame ambayo itaanza hivi karibuni na timu hizo zote zipo kundi moja kwenye nichuano hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video