Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm (kulia)
Michuano ya 40 ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, (Cecafa Kagame Cup) inayoshirikisha timu 13 mwaka huu inaanza kutimua vumbi leo jijini Dar es salaam.
Mashindano
haya ambayo yanashirikisha timu 13 mwaka huu yamedumu kwa muda mrefu, ila kwa
bahati mbaya yamekuwa na muonekana ule ule, hayana mvuto mbele ya mashabiki wa
soka.
Mechi za ufunguzi leo uwanja wa Taifa ni APR ya
Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan
saa 8 kamili mchana, KMKM ya Visiwani Zanzibar inaivaa Telecom ya Djibout
uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji Yanga wakiikaribisha Gor Mahia
kutoka Kenya saa 10 jioni.
Kuelekea mechi ya Yanga na Gor Mahia, kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema:
“Nimekuwa Afrika tangu mwaka 1996 hivyo nina uzoefu na soka la timu za hapa kwa muda mrefu, tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuikabili kila timu kwenye michuano hii. Kitu kikubwa ni kwamba, mimi huwa sidharau mpinzani wangu kwasababu kwenye soka lolote linaweza kutokea na hakuna mtu anayejua matokeo”, amesema Pluijm.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Gor Mahia, Mscotish Frank Nuttal amesema yeye hana uzoefu mkubwa na soka la Afrika ukilinganisha na mpinzani wake (Van Pluijm) lakini amesisitiza kuwa vijana wake wako vizuri kuikabili Yanga leo uwanja wa Taifa.
“Yanga ni timu kubwa japo sijawahi kuiona ikicheza lakini naamini ni timu yenye ushindani na mechi ya kesho itakuwa ngumu lakini mwisho wa mchezo tutajua matokeo”, amesema kocha huyo.
Kwa faida
yako msomaji, michuano ya mwaka huu ina makundi
matatu ambapo kundi A lina timu za Yanga
(Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar),
Khartoum-N (Sudan).
Kundi B
linajumuisha klabu ya APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi),
Heegan FC (Somalia).
Kundi C lina
timu za Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na
KCCA (Uganda).
0 comments:
Post a Comment