Saturday, July 25, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amefunguka kuhusu kumsugulisha benchi kiungo mshambuliaji wa timu hiyo kutoka Brazil, Andrey Coutinho.

Coutinho hakuwapo hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba wa Yanga wakati timu hiyo ya Jangwani ilipofungwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia katika mechi yao ya kwanza ya Kundi A la Kombe la Kagame Jumamosi iliyopita.

Mbrazil huyo anayesifika kwa upigaji wa faulo na kona zenye macho, alianzia benchi katika mechi ya pili ya kundi hilo Yanga iliposhinda 3-0 dhidi ya vibonde wa kundi, timu ya Telecom ya Djibouti, lakini akaingizwa dakika ya kwanza kati ya tatu za nyongeza na aligusa mpira mara moja kisha refa akamaliza pambano.

Hata katika mechi ya jana ambayo Yanga walishinda 2-0 dhidi ya KMKM, Coutinho aliingizwa dakika ya kwanza ya dakika tatu za nyongeza, lakini hakugusa mpira hata mara moja kabla ya refa Souleiman Djama kutoka Djibouti kupuliza kipenga cha mwisho.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mara tu baada ya mechi hiyo kumalizika, Pluijm alisema kuna siri ya kumsugulisha benchi mchezaji huyo.

"Ni kweli Coutinho amekuwa hapati nafasi katika kikosi chetu kwenye michuano hii ya Kombe la Kagame, lakini sitawaambia kwanini imekuwa hivyo. Kuna jambo tunaliangalia," alisema Pluijm.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video