Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wa pili wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2017.
Tanzania ambayo ipo nafasi ya mwisho katika kundi G lenye timu za Nigeria, Chad na Misri inatarajia kucheza na timu ya taifa ya Nigeria 'Super Eagles' September 5 mwaka huu ndani ya uwanja wa kisasa wa Taifa , Dar es Salaam.
Kwa upande wa Nigeria ambao wameonesha kujiimarisha zaidi kwa ajili ya mchezo huo, kocha wa timu hiyo Sunday Oliseh akiwa na siku kadhaa toka arithi nafasi ya kocha aliyetimuliwa Stephen Keshi ameanza kutaja nyota atakaowatumia kwa ajili ya mchezo huo.
Katika mipango ya Kocha Oliseh, kikosini anatajwa pia kuwepo kiungo wa Chelsea John Obi Mikel ambaye hakuitwa timu ya taifa ya Nigeria tangu November 2014, taarifa kutoka kwa afisa wa ngazi za juu za soka nchini Nigeria amevujisha stori ya kuitwa kwa Obi.
“Mikel bado anabakia kuwa moja kati ya nyota wa Nigeria wanaocheza Ulaya licha ya kuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara na Chelsea, hizo ndio sababu za Oliseh kumjumuisha katika mipango yake ya kuanza kuwania nafasi kufuzu kucheza AFCON dhidi ya Tanzania mwezi ujao… Mikel atacheza nafasi ya kiungo mkabaji kama anavyocheza akiwa na klabu yake” hii ni sehemu ya nukuu kwenye stori za Nigeria ambapo wanasema aliyetoa taarifa ni mmoja ya Viongozi wa juu kwenye Soka Nigeria japo hawakumtaja jina.
Nigeria ipo nafasi ya pili kwa point tatu katika msimamo wa kundi G nyuma ya Misri ambayo ina point tatu na magoli matatu baada ya kuifunga timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment