Tuesday, July 21, 2015

Kocha wa mkuu wa Khartoum National Club Kwesi Appiah akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati timu yake inacheza na Telecom ya Djibouti
Kwesi Appiah kwasasa anakinoa kikosi cha Khartoum National Club ya Sudan tangu Disemba 2014, huyu ndiye kocha pekee aliyefundisha timu ya Taifa iliyoshiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil kati ya makocha wengine 12 wanaovinoa vikosi vinavyo shiriki mashindano ya Kagame yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Alivyoanza ukocha:
Alihudhuria mafunzo ya ukocha kwenye vilabu vya England vya Manchester City na Liverpool. Baada ya hapo alikuwa kocha msaidizi wa Ghana kati ya 2007 na 2012. Mwaka 2011 alikiongoza kikosi cha vijana wa timu ya Taifa ya Ghana cha U23 kwenye michuano ya All Afrikan Games ambapo waliibuka washindi na kutwaa kombe hilo.
Kwesi Appiah 3Aprili 2014 aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, akiwa kocha wa Ghana, timu yake ilifanikiwa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil akiandika historia ya kuwa kocha wa kwanza mweusi kuipeleka timu ya taifa (Ghana) kwenye michuano ya kombe la dunia.
Kwesi Appiah 6Hata hivyo hakufanikiwa kufurukuta kwenye michuano hiyo mikubwa ya soka ulimwenguni kwani timu yake ilienguliwa kwenye hatua ya makundi lakini aliongezwa mkataba mpya Mei 2014 licha ya Ghana kusukumwa nje ya mashindano kwenye hatua ya mwanzoni.
Kwesi Appiah 4Septemba 2014 aliamua kubwaga manyanga kukinoa kikosi cha Ghana kwa makubaliano maalumu japo haikuwekwa wazi kwanini aliamua kuikacha timu hiyo.
Kwasasa anaifundisha timu ya Khartoum National Club ya Sudan akiwa kama kocha mkuu tangu mwezi Disemba mwaka 2014.
Appiah akiwa na benchi zima la ufundi la Khartoum National Club
Appiah akiwa na benchi zima la ufundi la Khartoum National Club
Alishawahi kucheza soka kwenye ngazi mbalimbali:
Enzi zake alikuwa anakipiga kama beki wa kushoto, amecheza kwenye klabu ya Asante Kotoko ya Ghana kuanzia mwaka 1983 hadi 1993.
Appia pia alicheza kwenye timu ya taifa ya Ghana kati ya 1987 na 1992 na amewahi kuwa nahodha wa The Black Stars.
Kwesi Appiah 7Kuhusu michuano ya Kagame:  
Appiah amesema alikuwa anasikia kuhusu michuano ya CECAFA inayohusisha timu za taifa na vilabu.
“Nilikuwa natamani sana kujua michuano hii kwa kushiriki moja kwa moja nikiwa na timu yangu  ya Khartoum”, alisema.
“Tunacheza dhidi ya timu kubwa kwenye kundi letu lakini ukitaka kuwa kwenye upande mzuri hupaswi kuhofia kukutana na timu ngumu”, alisema kwa kujiamini.
“Sipo kwenye michuano ya CECAFA ili kukutana na timu ngumu au dhaifu, hakuna kitu kama hicho, hakuna timu dhaifu. Timu zote zinacheza vizuri kwasasa”, alisisitiza.
“Tunashiriki mashindano haya kwa lengo la kuangalia kikosi chetu pamoja na wachezaji kwa ajili ya mashindano mengine yajayo”, aliongeza.
“Ushiriki pia ni muhimu kwa wachezaji kwasababu inanyanyua hadhi ya wachezaji na timu kwa ujumla. Tumekuja Tanzania tukiamini kwamba sisi ni timu nzuri”, alimaliza.
Kwesi Appiah
Taarifa kwa ufupi kuhusu Appiah:
Jina kamili: James Kwesi Appiah
Tarehe ya kuzaliwa: 30 Juni, 1960 (mika 55)
Sehemu alikozaliwa: Kumasi, Ashanti, Ghana
Nafasi aliyokuwa akicheza: Beki wa kushoto
Timu alizocheza: Asante Kotoko (1983-1992), timu ya taifa ya Ghana (1987-1992)
Nafasi yake kwa sasa: Kocha mkuu wa Khartoum Naional Club (Sudan)
Timu alizowahi kuzifundisha: 2011 (Ghana U23), Ghana (2012-2014), Khartoum (2014-hadi 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video