Wednesday, July 22, 2015

Wachezaji wa Khartoum wakishangilia goli

Mabingwa wa Zanzibar, KMKM wamepoteza mechi ya pili katika michuano ya Kagame baada ya kuchapwa 2-1 na Khartoum National Club ya Sudan.
Mabao ya Khartoum yamefungwa na Salah Eldin Osman Bilal dakika ya saba kipindi cha kwanza wakati goli la pili likifungwa na Antony Akumu Agay dakika ya 84,  huku goli pekee la KMKM likitiwa kambani na Mateo Antony Saimon dakika ya 58.
Mechi iliyopita ya kundi A, KMKM walifungwa 3-1 na mabingwa mara tano wa mashindano hayo, Gor Mahia ya Kenya.
Hata hivyo, KMKM walishinda 1-0 kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Telecom ya Djibout.
Hatima ya KMKM ipo kwenye tundu la sindano kutegemeana na matokeo ya mchezo unaondelea muda huu kati ya Yanga na Telecom.
Yanga walianza vibaya mechi ya ufunguzi kwani walikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video