Tuesday, July 14, 2015


Golikipa Hugo Lloris wa klabu ya Tottenham Hotspur ya jijini London, ameipa pigo klabu yake ya Spurs baada ya kuumia katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu England.

Nahodha huyo wa Tottenham Hotspur amevunjika mifupa ya kiganja cha mkono katika mazoezi ya awali na 'preseason' na klabu yake.

Golikipa huyo raia wa ufaransa, anatarajiwa kuukosa mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford mwezi ujao wa Agosti.

Pamoja na kuwa ni pigo kwa Spurs lakini taarifa hizi sio pia nzuri kwa Manchester United ambao wanawania saini ya mlinda mlango huyu hasa kutokana na kutokuwa na uhakika wa mustakabali wa kipa wao David de Gea anayewindwa na Real Madrid.

Katika hali ya sintofahamu, golikipa De Gea amejumuishwa katika safari ya preseason na wenzake nchini Marekani huku fukuto la kutakiwa na Madrid likiwa linaendelea chinichini.


Aidha golikipa mwenza wa Manchester United, Victor Valdez ameachwa katika safari hiyo bila ya taarifa zozote kutolewa. Hali hiyo inatokea wakati klabu za nchini Uturuki zikimwania Valdez ambaye alitamba na klabu ya Barcelona kwa misimu 13 kabla ya kuumia na kisha kuondoka akiwa huru.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video