MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza ametua jijini Dar es Salaam muda mfupi uliopita kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kujiunga na mabingwa mara 18 wa Tanzania Bara, Simba.
Kiiza aliyetemwa Yanga Desemba mwaka jana kumpisha mshambuliaji Mliberia Kpah Sherman, ametua jijini hapa akifuatana na kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda mwenzake, Simon Sserunkuma.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Rais wa Simba jana, Kiiza atapimwa afya na iwapo akifuzu, atapewa mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Msimbazi.
0 comments:
Post a Comment