Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
BAO pekee la mshambuliaji lililofungwa na mshambuliaji Ivan Sserunkuma limetosha kuipeleka KCC robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame baada ya muda mfupi uliopia kutoka kifua mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Malakia FC.
Sserunkuma amefunga bao hilo dakika ya 12 akimalizia kwa shuti la mguu wa kushoto krosi iliyotua ndani ya sita kutoka wingi ya kulia.
Kwa matokeo hayo, KCC wamemaliza hatua ya makundi wakiwa na pointi sita katika Kundi C linaloongozwa na Azam FC ambao kwa sasa pia leo wanakipiga dhidi ya Adama City ya Ethiopia.
KCC sasa itasubiri mshindi wa pili katika Kundi A ambalo lina timu za Al Khartoum , Gor Mahia na Yanga ambazo tayari zimeshafuzu inagawa bado zina mechi moja kila moja mkononi.
0 comments:
Post a Comment