Saturday, July 25, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
BENCHI la ufundi la KCCA FC ya Uganda limefanya mabadiliko ya wachezaji watano katika kikosi chake cha kwanza kitakakachovaa Malakia FC kwenye Uwanja wa Taifa leo saa 8:00 aklasiri katika mechi ya mwisho ya Kundi C kuwania kuingia robo fainali ya Kombe la Kagame.

Timu zote mbili zinasaka tiketi ya kuifuata Azam FC ya kundi hilo iliyofuzu kuingia robno fainali ya michuano hiyo baada ya kushinda mechi mbii za awali za hatu ya makundi.

Mabadiliko hayo ya KCC FC yamewakumba Denis Okot ambaye nafasi yake imechukuliwa na Sakka Mpiima katika nafasi ya beki wa pembeni kulia, Martin Mpuuga abarejea kuziba nafasi ya kinda Timothy Awany wakati Isaac Sserunkuma anachukua nafasi ya majeruhi Derrick Nsibambi.

Mabadiliko mengine ya mabingwa hao wa Uganda yanamgusa msgambuliaji wa zamani wa Yanga, Shaban Kondo na Hakim Ssenkumba ambao wanaanza leo kuziba nafasi za Muzamir Mutyaba (majeruhi) na Dan Nsubuga.

Beki Farouk Matovu na kiungo Owen Kasule pia wanaanzia benchi baada ya kukosekana katika mechi iliyopita waliyoshinda 1-0 dhidi ya Adama City kwenye Uwanja wa Karume jijini hapa Julai 22.

KCC inahitaji ushindi au sare katika mechi ya leo ili ifuzu hatua inayofuata ya nane bora.

Kikosi cha KCC FC Kinachoanza leo kina: Emmanuel Opio (Kipa), Denis Okot, Joseph Ochaya, Martin Mpuuga, Hassan Wasswa, Hakim Ssenkumba, Ivan Ntege, Shaban Kondo, Tom Masiko, Isaac Sserunkuma na Michael Birungi.

Benchini wapo: Benjamin Ochan (Kipa), Farouk Matovu, Sakka Mpiima, Owen Kasule, Timothy Awany, Habib Kavuma na Dan Nsubuga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video