Thursday, July 23, 2015

Rais wa TFF, Jamal Malinzi

Kwa kiasi kikubwa Sasa hivi Tanzania imebaki nzuri katika ramani, pale inapoonekana imezungukwa na kubarikiwa na rasilimali mbalimbali, hata nyimbo ya kipindi hicho ambayo hata babu yangu aliimba nayo ilisema hivyo, ukitazama ramani utakutana na nchi nzuri haswa.
 Kuna wakati unaamua kuweka lawama upande wa kushoto maana hazina tija tena Kisha utafute wa kufanya naye kazi nzuri, lakini tatizo limebaki kuwa kila mmoja amegubikwa na tamaa ya kulitendea taifa uhalifu. 
Tunaiba rasilimali zake, tunawaongopea wananchi wake, na tunaliweka mwisho katika kila sekta. Hata asiyenacho anakuwa nacho mbele yetu,  jirani yetu anaamua tu na kusema mimi ndio mzalishaji bora wa Tanzanite, mwingine anaamua na kusema samaki wa ziwa nyasa wote ni wangu,  Kisha na kwenye soka Kuna majirani wanasema jina la Lunyamila ni letu, wanawaita watoto wao na kulitukuza. Kwetu sisi ni sawa tu,  Kenya wakifurahia utajiri wa Tanzanite,  Malawi wakila samaki wa Nyasa na Waganda wakilifurahia jina la Lunyamila kuliko sisi wala haitupi shida. Itatupaje shida wakati hata TFF wanaamini suluhisho la matatizo ni kuwa na kamati nyingi kuliko utendaji sahihi na stahiki.
 Itatupaje shida wakati Ile nchi nzuri kwenye ramani watu wake wanaibadili kwa lazima. Ukimuuliza kila mtu atakwambia ni siasa,  lakini kwani ni Tanzania pekee yenye siasa au maana ya siasa ni ipi? 


Tanzania ndio nchi pekee ambayo siasa ni uongo na sio ahadi,  siasa ni ubadhilifu na sio utendaji kusudiwa na siasa ni unafki na sio ukweli. Ndio maana jibu letu jepesi katika kila swali gumu hata uchumi ni siasa. Silipendi kweli.  
Wakati mheshimiwa Rais wa TFF akiingia madarakani nilipata kukishuhudia kitabu chake cha ahadi,  ni kurasa mbili tu za mwanzo ambazo zingeweza kukufanya uamini naye alikuwa na mlengo wa kisiasa ya Tanzania. Sina tatizo na hilo, ila nina tatizo na anachokifanya. Kaufanya ulimi ufanye kazi ya mikono na mikono inafanya kazi ya ulimi. Hakuna utekelezaji. 
Anachoshika ndicho anachokiacha na anachokifuata ndicho anachokipita. Hajajua anataka nini,  na hajafikiria aanze na kipi. Malengo ya Taifa Stars maboresho yamefikiwa kwa kiasi gani?  Mlengo wa vijana na soka lao upo wapi?  Hadhi ya vijana katika soka imekwenda wapi? Aliahidi kusimamia vijana kama wale wa copa coca Cola waliofika Brazil na kuchukua Kombe lakini ni kwa mikakati ipi? Hii ya kupanga kamati za ligi na viwanja pekee au ule wa kufurahia kuonyeshwa kwa ligi?  Dhambi ni kunipa chakula nile kisha kumbe kibichi, ni kama dhambi ya kunionyesha mpira wa taifa ninalolipenda kwenye TV Kisha likaniliza nyumbani kwangu kwa kukusudia.
 Hakuna njia fupi katika mafanikio yoyote. Na hakuna nchi iliyoendelea pasi na kuwekeza vyema katika sekta yoyote. Tumeamua kujipa upofu ilhali mwanga ukipenyeza unatuumbua kuwa tunaona vyema. Tumeshindwa hata kukumbuka mashuka kukiwa kumekucha, asubuhi inatukuta vile vile,  giza linawadia tuko vile, na kisha 2017, 2018 mpaka 22 zitatukuta hivyo hivyo.
Tumeweka chuki dhidi ya maandalizi, tumehama dunia ya kisasa tunaitafuta inayotufaa sisi peke yetu. Mwarobaini pekee wa soka la nchi yoyote ni uwekezaji kwa vijana, na kubadili muonekano mzima wa utendaji kazi wa Chama cha soka na washirika wake. 
Mabadiliko yatakuja kwa mipango sahihi. Siku ambayo tutasahau mipango ya ghafla (crush program) kama za maboresho na kuingia mikoani na kubadili muonekano mzima wa uongozi na utendaji wa vyama vya soka huko,  kuweka ligi za vijana za vilabu zenye udhamini stahiki na kurushwa katika vituo moja kwa moja, tusimamie hadhi za Copa coca Cola,  Uhai na Rolling Stone, kuweka usimamizi au mkono wa TFF katika mashindano yenye usimamizi tayari ya UMISSETA kitu ambacho Taifa haliwezi kuwanyima ruksa hiyo,  kubadili mfumo mzima wa Chama cha soka. Nani alisema msururu wa watu katika ofisi ambayo kimsingi ni ndogo ndo kutaleta tija kwa soka letu? Tuweke nguvu katika wachezaji vijana katika timu ya Taifa,  utegemezi wa Haroub na Yondani ambao binafsi hata Yanga walitakiwa waanze kuondoa tuhimize. 
Kama vyama vya soka vya mikoa vimejaa ubabaishaji ambao TFF haiutizami unategemea maendeleo yapi? Kama wachezaji na vilabu hawana maelewano ya kimikataba na haki zao na TFF inamaliza kiurafiki utatoa wapi maendeleo?


Hakuna mti uliosimama vyema ikiwa mizizi yake imesinyaa. Bahati mbaya sana ni kuwa kwetu hivi hatuoni umuhimu wake, tunawaza makubwa wakati madogo tunayapiga teke, tumeamua kuamini katika John Boko na sio kuwaandaa akina Hajib. Halafu tunasema tumepewa tiketi ya kuandaa michuano ya vijana. Unawasha moto mahala palipo lowanishwa na maji ya mvua? Hapana sharti upakaushe kwanza. Ni ngumu kumlea mke usiyempenda kwa dhati.  Huwezi kuwa kiongozi makini kama unaomba kuandaa mashindano ambayo wewe huyatilii mkazo. Sipingi uamuzi wa kuandaa mashindano, lakini mipango yake inatakiwa iambatane na mazingira rafiki na madhubuti ya kunufaika na mashindano hayo.  Kila nikitizama ahadi za mheshimiwa Rais nachelea kusema kuwa walau kurasa zake mbili za mwanzo hajazitimiza. 
Sihitaji kukumbuka kurasa zilizosalia. Kama hata jezi za timu ya Taifa hazitambulishwi na wachezaji bali wadau napata shaka na wapi tunaelekea. Tungejichimbia shimo wenyewe angalau, lakini mashimo haya tumewawekea mpaka wajukuu wetu yawameze. Tanzania yetu sio nzuri tena, hata kwenye ramani imepoteza mvuto, ningekuwa na uwezo ningeibadili ramani. Nyimbo aloimba babu yangu kwa usahihi,  inaimbwa leo na vitukuu vyake kimakosa.
Ahsanteni.
By Nicasius Nicholaus Agwanda ( Nicasius Coutinho Suso)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video