Friday, July 31, 2015

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Michuano ya 40 ya Cecafa Kagame Cup 2015, Ijumaa hii itachezwa michezo miwili ya nusu fainali, kisha ' tamati' yake itafikia Jumapili kwa michezo ya fainali na ule wa kutafuta washindi wa tatu na Yule wa Nne.



Jumla ya gemu 22 zimekwisha chezwa, mechi ya 23 itawakutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya na Al-Khartoum ambazo awali zilikutana katika mchezo wa kundi A na kutoa matokeo ya 1-1. Gor wanasotea taji la kwanza kwa miaka 30 sasa wanakutana na timu yenye mbinu kali za kushambulia.
Khartoum ambayo ilipewa nafasi ya waliokuwa mabingwa wa mwaka uliopita, Al Marreikh haikutajwa kama moja ya timu zilizo na uwezo wa kutwaa ubingwa mwaka huu lakini ilishangaza zaidi baada ya kuwachapa washindi wa pili wa michuano iliyopita, APR ya Rwanda kwa mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali.
Timu zote mbili, Gor na Khartoum zimekuwa na tabia ya kucheza mipira ya juu kutokana na maumbo na urefu wa wachezaji wa timu hizo. Nahodha wa Khartoum anasaka kiatu cha pili cha ufungaji bora wa Cecafa amefunga mara nne katika gemu tano za timu yake huku kiungo-mshambulizi, Masiko akiwa amefunga magoli mawili.
Gor Mahia ambayo haijapoteza katika michezo 23 mfululizo ( michezo 18 ya ligi kuu Kenya na mingine mitano katika Kagame Cup) imefunga jumla ya magoli 11, manne yakiwa yamefungwa 'gumzo la michuano', Michael Olunga na mengine mawili yamefungwa na kiungo wa kushoto, Geofrey Walusimbi wakati walipoisha Al Shandy 2-1 katika mchezo wa robo fainali siku ya Jumanne.
Mabao 66 yamefungwa hadi sasa na kikosi cha Khartoum ndiyo kinaongoza kwa kufunga katika michuano ya mwaka huu, chini ya kocha Mghana, Akwessy Appiah timu hiyo ya Sudan Kaskazini imefunga jumla ya magoli 14 katika michezo mitano. Ilifunga magoli 10 katika mechi nne za makundi na ndiyo timu iliyofuzu nusu fainali kwa ushindi mkubwa zaidi zaidi.
Sare ya 0-0 iliendeleza kiwango cha juu katika ulinzi, iliwabana sana Yanga na kujaribu kufunga mara kadhaa, kikosi cha Muingereza, Stewart Hall kimefunga jumla ya magoli 8 katika michezo minne iliyopita. KCCA ilichapwa 1-0 na Azam FC katika mchezo wa kundi C ilifuzu robo fainali ikiwa imefunga mara mbili tu katika michezo mitatu ya makundi lakini, iliweza kuchomoa makucha yake na kuitandika 3-0 Al Malakia katika robo fainali.
Mechi kati ya wawakilishi pekee wa Tanzania, Azam FC na KCCA ya Uganda inataraji kuwa ngumu kufungika kwani timu hizo ndiyo zilizounga magoli machache miongoni mwa timu nne zilizofuzu nusu fainali. Azam ilifuzu kwa nusu fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penalti dhidi ya Yanga SC siku ya Jumatano. Timu hiyo ya Uganda ilishika nafasi ya 3 katika michuano ya Kigali, Rwanda, 2014 imekuja Dar es Salaam ikiwa na baadhi ya wachezaji wazoefu lakini kundi kubwa ni wachezaji vijana. Imeshindwa kufunga katika mchezo mmoja tu dhidi ya Azam FC lakini ni ngumu pia kufungika kama ilivyo kwa Azam ambayo haijaruhusu goli lolote.
KCCA inaweza kuwaanzisha nyota hawa 11; Emmanuel Opio (GK), Denis Okot, Habib Kavuma, Hassan Wasswa, Timothy Awany, Tom Masiko, Ivan Ntege, Hakim Ssenkumba, Isaac Sserunkuma, Muzamiru Mutyaba, Joseph Ochaya. Si timu ya kubeza.
Magoli kumi yalifungwa katika michezo minne ya robo fainali. Magoli 56 yalifungwa katika michezo ya hatua ya makundi, hiyo inaonesha wazi kuwa michuano imekuwa na magoli ya kutosha na timu nne zilizo nusu fainali zimefunga jumla ya magoli 38. Mu-Ivory Coast, Kipre Tchetche ndiye anaongoza kuifungia Azam FC katika michuano hii. Kipre amefunga magoli matatu katika gemu nne wakati 'patna'wake katika safu ya mashambulizi, John Bocco amefunga mara mbili.
Wengi wanataraji kuona fainali ya GOR na AZAM lakini namna timu nyingine mbili zinavyocheza unaweza kutazama fainali ya Khartoum na KCCA. Soka si mchezo wa kutabirika kirahisi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video