Na Frank Mgunga
Aliyewahi kuwa kocha wa klabu ya Afrikan sports ya jijini Tanga ambayo imepanda daraja kucheza ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, John William maarufu kama Del Piero ametua katika klabu ya Coastal Union 'wagosi wa kaya wagosi" na kusaini mkataba wa miaka minne kukinoa kikosi cha U20 cha klabu hiyo.
Del Piero ameiambia MPENJA SPORTS kwamba tayari ameshasaini mkataba huo na anaishukuru klabu hiyo kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kurudi tena jijini Tanga baada ya kutoka Geita alipokuwa akiendeleza kipaji chake cha kuinua vipaji vya vijana wadogo.
"Naishukuru sana klabu ya coastal union kwa kuona mchango wangu katika mchezo wa soka tangu nikiwa na klabu ya African sports kabla ya kuelekea Geita na sasa nimerejea tena jijini Tanga kuifundisha coastal union kikosi cha U20," alisema Del Piero.
Hii inachukuliwa kama upinzani wa hali ya juu unaotengenezwa na klabu mbili za Coastal Union na African Sports zote za jijini Tanga ambazo zinaendelea kujiimarisha kwa ajili ya mitanange ya ligi kuu soka Tanzania Bara msimu 2015/2016.
0 comments:
Post a Comment