Tuesday, July 28, 2015

Na Simon Chimbo;
Raheem Sterling ni moja kati ya majina yaliyotajwa zaidi katika dirisha hili la usajili wa kiangazi barani ulaya. Tofauti na pengine wakati mwingine, sakata la Sterling lilileta hisia mchanganyiko miongoni mwa mashabiki.
Waswahili husema, 'tuweke akiba ya maneno'. Hatimaye Raheem akavunja rekodi ya ada ya uhamisho wa klabu ya Manchester City kwa uhamisho wa pauni 49m kutoka Liverpool.
Safari ya Raheem ya kuondoka Liverpool hadi Manchester City, ilimuweka katika wakati mgumu sana kijana huyo pamoja na familia yake, mchumba wake alibaguliwa rangi na mashabiki wa Liverpool huku Raheem akizomewa na kutukanwa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Pamoja na wengi kubeza uwezo wa kijana huyo lakini mimi siamini hilo hata nusu. Kama Sterling angekuwa mchezaji wa kiwango cha kawaida, mashabiki wa Liverpool wasingeonesha hasira zao tangu Raheem atangaze kuihama klabu hiyo.
Lakini pia, hata kama wachezaji wa kiingereza huuzwa kwa bei ghali, Manchester City wasingetoa pauni 49m kwa Raheem kama angekuwa ni wa kawaida kama wengi tunavyombeza.
Wiki iliyopita, akiichezea kwa mara ya kwanza klabu yake mpya ya Manchester City, mashabiki wa Liverpool walianza kumzomea kwa nguvu wakati tu akitoka vyumbani.
Mario Baloteli akaandika ujumbe katika Twitter yake kuwaomba mashabiki wa klabu yake ya Liverpool kuacha kumshambulia kijana huyo mdogo mwenye kipaji na badala yake kumsapoti kama ambavyo hufanya siku zote.
Nimenukuu usemi wa kiswahili usemao, 'tuweke akiba ya maneno'. Katika mechi hiyo dhidi ya Roma wakati akizomewa kwa nguvu zote na mashabiki, Raheem akafunga goli ndani ya sekunde 137 tu ya mchezo.
Mario Baloteli akatwiti tena kwamba, "Safi Raheem, njia nzuri ya kuwanyamazisha wanaokubeza".... pamoja Baloteli pia alipata matusi kutoka kwa mashabiki hao lakini ujumbe ulifika.
Ninachokiamini, ni kwamba mtu huumia sana anapoondokewa au anapopoteza kitu kizuri na muhimu kwake. Hii ndio inawaumiza Liverpool.
Wapo wanaosema Sterling atafulia kwenye kikosi hicho cha Manuel Pellegrine lakini tunakubaliana sote kwamba dalili ya mvua ni mawingu, Sterling kafunga tena magoli mawili dhidi ya Vietnam11 bila shaka ni mwanzo mzuri sana.
Sioni sababu za Sterling kufeli akiwa City. Raheem sio mgeni na ligi ya hii, Raheem alikuwa akicheza na wachezaji wengi wenye uwezo wa kati wa Liverpool, lakini alikuwa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Brendan Rodgers.
Mara nyingi ukikaa na wahuni, ni rahisi nawewe kufuata tabia hizo, lakini pia ukikaa na wastaarabu utavuna tabia hizo.
Manchester City ina wachezaji wengi wa kiwango cha juu zaidi na hili litamuwezesha Sterling kujifunza na kuongeza zaidi alipo sasa na kusonga mbele.
 Bila shaka Sterling atakuwa na assists nyingi kwa kuwa atakuwa akimpasia Sergio Aguero pale City. Lakini pia nyuma ya Sterling yuko Yaya Toure, Fernandinho kitu kitakacho mpa fursa za kushambulia zaidi kuliko kuhofia kuzuia.
Sterling atataka kuwakosoa wanaobeza kipaji na uwezo wake na hivyo atajituma zaidi na mwishowe tutakaa kimya.
Samir Nasri alitukanwa sana na mashabiki wa Arsenal wakati akiondoka kuelekea City lakini mwisho wa msimu akatwaa kikombe cha ubingwa wa ligi na akawatambishia waliokuwa wakimtukana.
Naliona hilo pia kwa Raheem Sterling. Matusi yetu na kebehi kwa Raheem zitatugeukia siku analinyenyua kombe la ubingwa na klabu yake ya Manchester City, tuweke akiba ya maneno.
Inawezekana pia Raheem Sterling asing'ae katika kikosi hiki cha City, lakini sio sababu za kumpiga mawe na kumzomea ama kuja kunitukana mimi, na ndio maana nasisitiza tuweke akiba ya maneno.
Aidha kwa Liverpool nafikiri wanahitaji kufuatilia vizuri zaidi maendeleo ya kikosi chao kuliko kumsakama Raheem. Kuna wanaoamini Liverpool imeramba dume kwa kupata mkwanjwa mzito kwa mauzo ya Sterling mwenye miaka 20.
Bila shaka Roberto Firmino ni usajili mzuri na ataziba kabisa pengo la Raheem Sterling katika kikosi hicho cha Merseyside, tunasubiri kuona.
Tujifunze kuwajaji wachezaji kwa vigezo na sio hisia. Mashabiki wa Manchester United waliamini Angel Dimaria angeshaini katika kikosi chao lakini sasa anauzwa, tuweke akiba ya maneno.
Asalam Aleikum.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video