Man United wakitua jana San Jose
Klabu ya San Jose Earthquakes inagawa bure jezi za Manchester United kwa mashabiki wanaonunua tiketi za kuangalia mechi yao ya kesho dhidi ya kikosi cha Louis van Gaal kilichopo ziarani Marekani kujiandaa na msimu mpya.

Tiketi za mechi hiyo bado zinauzwa ili kujaza uwanja wa Avaya ambao utatumika kesho na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Marekani inawashawishi zaidi kwa kugawa jezi ya nyumbani ya Manchester United kwa wale wanaonunua tiketi mbili au zaidi.

Nyota wa Manchester United walitua jana San Jose kwa ndege binafsi.

Mashabiki waliofika jana kwenye ofisi za klabu na kununua tiketi mbili au zaidi walipewa jezi hizo, ingawa zitapita muda wake siku chache zijazo kwani Man United watatumia jezi za Adidas msimu ujao.
Jezi ya sasa ya Nike inaisha muda wake Julai 31 mwaka huu,.
Baada ya mechi dhidi ya Earthquakes, United watacheza na Barcelona siku ya Jumamosi katika uwanja wa Levi, nyumbani kwa San Francisco 49ers .
Uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 68,500 upo mjini Santa Clara ambapo ni karibu ni uwanja wa mazoezi.
0 comments:
Post a Comment