Timu ya Lyon kupitia Rais wa klabu hiyo ya Ufaransa, Jean-Michel Aulas amesema mchezaji wao Alexandre Lacazette hataondoka klabuni hapo kwa dau dogo la usajili.
Aulas amesema watakuwa tayari kumuachia kama kuna timu itafika na ofa ya pauni milioni 35, chini ya hapo hawatakubali kuondoka Ufaransa.
Lacazette(24), anahusishwa na mipango ya kuhamia timu ya Arsenal na Liverpool msimu huuu.
Aulas amesisitiza watamruhusu kuondoka mchezaji huyo kama watapata dau zuri.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Ufaransa amefunga magoli 27 msimu ulioisha wa Ligue 1 na Lyon.
0 comments:
Post a Comment