Tuesday, July 28, 2015

Michezo ya robofainali ya Kagame Cup inaanzakutimua vumbi leo kwenye uwanja wa Taifa , hapa tumekuwekea namna ambavyo timu zinazocheza robofainali zilivyokata tiketi ya kucheza robo fainali kutoka kwenye makundi zilikokuwa zimepangwa.
Timu ya Yanga ilianza vibaya michuano hii kwa kukubali kipigo cha goli 2-1 mbele ya wababe wa soka la Kenya timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi uliopigwa Julai 18 katika uwanja wa Taifa. Yanga walianza kufunga goli lao kupitia kwa Donald Ngoma lakini goli hilo lilisawazishwa na Gor Mahia na baadae timu hiyo kuongeza bao la pili na kuibwaga Yanga.
Yanga ilizinduka kwenye mchezowake wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-0 mbele ya Telecom ya Djibouti anbayo ilionekana kuwa kibonde kwenye kundi A kwa kumaliza bila pointi huku ikifungwa idadi kubwa ya magoli ambayo ni magoli 12. Mechi iliyofuata ambayo ilikuwa ni ya tatu, Yaga ilipata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya KMKM ukiwa ni ushindi wake wa pili na kujihakikishia kucheza hatua ya robo fainali baada ya kufikisha pointi sita.
Mechi ya mwisho kwenye kundi A Yanga ilishinda kwa goli 1-0 ilipochuana na wakali wengine wa kundi hilo timu ya Khartoum ya Sudan na kufanikiwa kumaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye kundi A nyuma ya Gor Mahia ya Kenya.
Kwa upande wa Gor Mahia, hii ni timu ambayo imeonekana kuwa tishio kwenye michuano hii kwani haijapoteza hata mchezo mmoja kwenye kundi lake ambalo ni Kundi A. Ilianza kwa kuifunga Yanga 2-1 kwenye mchezo wa ufunguzi, halafu ikaitandika KMKM kwa goli 3-1 kwenye mchezo wake wa pili. Mechi ya tatu Gor Mahia ilikutana na Khartoum National Club ambapo mchezo huo ulimalizika kwa mimba hiyo kutoka sare ya kufungana goli 1-1.
Mchezo wa mwisho kwa Gor Mahia, waliandika ushindi wao wa tatu na kuongoza kundi A baada ya kuifunga Telecom kwa jumla ya goli 3-1.
Timu ya Khartoum ni moja ya timu ambazo zilikuwa hazipewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kagame lakini walidhihirisha wao ni bora kufuatia kuicharaza Telecom kwa goli 5-0 kwenye mchezo wao wa kwanza. Khartoum iliandikisha ushindi wake wa pili ilipokutana na KMKM ambapo KMKM ililala kwa bao 2-1.
Khartoum inayonolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appia ambae aliiongoza Ghana kwenye fainali za kombe la dunia zilizofanyika Brazil mwaka 2014, timu yake ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Gor Mahi na ikapoteza mchezo wake wa mwiso ilipofungwa na Yanga kwa goli 1-0.
Azam FC ilifanikiwa kushinda mechi zake zote kwenye kundi lake (kundi B), mchezo wa kwanza Azam ilishinda kwa goli 1-0 dhidi ya KCCA ya Uganda. Mchezo uliofuata Azam ikaendeleza ubabe na kujihakikikishia kucheza robofainali ya Kagame kwa kushinda mbele ya Malakia FC ya Sudan Kusini kwa goli 3-0 na mechi yake ya mwisho Azam ikatoa kipigo kikali cha goli 5-0 ilipokutana na Adama City ya Ethiopia.
KCCA ya Uganda baada ya kuangukia pua kwenye mehi yake yake ya kwanza dhiddi ya Azam FC kwa kukubali kichapo cha goli 1-0, ililazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na Adama City kwenye mchezo wake wa pili. Kwenye mechi yake ya tatu ambayo ilikuwa ni ya mwisho kwenye kundi C, KCCA ikaibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Malakia FC na kukata tiketi ya kucheza robo fainali ya Kagame.
Timu nyingine iliyofuzu kucheza robo fainali ya Kagame mwaka 2015 ni APR FC ya Rwanda ambayo ni wakongwe wengine kwenye mashindano haya, APR ilianza Kagame kwa kushinda mchezo wake wa kwanza kwa kuifunga Al Shandy ya Sudan kwa goli 1-0. Mechi iliyofuata APR ilishinda kwa goli 2-0 dhidi ya timu ya Heegan kutoka Somalia. APR ilijihakikishia kucheza robo fainali ya Kagame mwaka huu kwa kuifunga LLBA ya Burundi kwa goli 2-1 na kuwa timu nyingine iliyoshinda mechi zake zote kwenye kundi ukiachilia mbali Azam FC.
Al Shandy nayo imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa kutoka sare ya kufungana kwa goli 2-2 kwenye mchezo wake dhidi ya LLBA ya Burundi baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa goli 1-0 mbele ya APR. Mchezo uliowapa nafasi Al Shandy nafasi ya kucheza robo fainali ni ule ulioikutanisha na timu ya Heegan ya Somalia na Al Shandy ikafanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-2.
Timu ya Malakia FC ya Sudan Kusini ni timu inayokamilisha timu nane zilizofuzu kucheza robofainali baada ya timu hiyo kutinga kwenye hatua ya robofainali kwa nafasi ya best loser kufutia timu hiyo kuwa na pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Adama City.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video