Na Simon
Chimbo;
Kwa wengi
nchini Argentina, soka ni moja ya vitu wanaviabudu sana. Katika jimbo
alilozaliwa mshambuliaji Carlos Tevez, Buenos, ndipo lilipo kanisa la gwiji wa
soka duniani, Diego Armando Maradona.
Kanisa hili
lilianzishwa na watu watatu Hernan Amez, Alejandro Veron na Hector Campomar
mwaka 2001.
Kanisa hili
limepata umaarufu mkubwa sana duniani kote huku likiwa na Tovuti yenye wafuasi
katika nchi za Hispania, USA, Mexico, Afghanistan na Ufilipino.
Hili ni
kanisa ambalo waumini wake humuabudu gwiji huyo Diego Armando Maradona na
kwamba ndio Mungu wao.
Waumini wa
kanisa hili, hufika kanisani hapo na kuanza kumuomba gwiji huyo kama Mungu wao
huku kukiwa pia na sala zinazomtaja Diego Armando Maradona.
Katika ibada
za kawaida, badala ya kutumia biblia, makasisi huwasomea kitabu ya historia ya
mchezaji huyo, 'Autobiography'.
Wakati wa
sherehe za misa kama ndoa, ubatizo na mambo mengine hufanyika siku ya kuzaliwa
Diego Maradona yaani October 30. Hii ni siku kubwa sana kwa wafuasi wa dini hii
duniani kote.
"Ni
muhimu kumuonesha mapenzi, 'El Diego' kutokana na miujiza mingi tuliyoipata
kupitia jina lake" anaeleza kasisi Amez mmoja wa waanzilishi wa kiroho wa
kanisa hilo miaka kadhaa iliyopita.
Katika jengo
hilo la kanisa, kuna alama za 'D10S' ambapo 10 ni utambulisho wa jezi namba aliyokuwa
akivaa enzi zake uwanjani, lakini linatengeneza neno kama Dios ambalo humaanisha
'Mungu' kwa lugha ya kihispaniola.
Amez ambaye
ni Padre wa kanisa hilo anamzungumzia Lionel Messi kama mmoja wa wanasoka adimu
duniani na kummwagia sifa kibao huku akitoa siri kwamba Messi alikua ni moja
kati ya watu wa kwanza kufika kanisani hapo kuchukua jezi iliyosainiwa na 'Mungu'
Maradona na kisha kuipeleka Barcelona.
"Watu
wote hupita mitaani kote tukikumbatiana na kushangilia. Tunasahau tofauti zetu
zote za kisiasa na kijamii kumtukuza El Diego. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kutuunganisha
kama Maradona"- anaeleza padri huyo Amez wa kanisa hilo.
Tarehe nyingine
muhimu ni 22 June ambapo huifanya kama ndio Pasaka katika kanisa hilo. Siku
hiyo ni siku ambayo mfalme huyo wa soka duniani, alifunga goli la mkono dhidi
ya England katika fainali za kombe la dunia mwaka 1986.
Bwana Amez
anasema goli na siku hiyo haitosahaulika sio tu duniani bali na mbinguni.
Lakini baada
ya kukosolewa vikali na baadhi ya watu na dini mbalimbali ulimwenguni kote
kuhusiana na kanisa hilo, padri Amez anakuja na utetezi huu, "sisi
hatuingiliani na dini zingine za ukristo. Tunamuabudu Maradona katika soka tu
na sio vinginevyo. Wengi wetu hapa ni waumini wa kanisa katoliki lakini kuhusu
soka, El Diego ndio 'mungu' wetu".
Inaelezwa
kuwa mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na England, Gary Linekar ambaye ni
mchambuzi maarufu wa soka hivi sasa pamoja na kocha wa Tottenham Hotspur,
Mauricio Pochettinho ni waumini na wanakadi za uumini wa kanisa hilo.
KIPI KINAVUTIA
HAPA?
Wakati
waumini wakiabudu kanisani, El Diego mwenyewe huwa akifanya shughuli zake ikiwa
hata kunywa bia na mambo mengine kwa kuwa yeye sio mchungaji wa kanisa hili bali
yeye ni 'mungu' hivyo waumini wanawajibu wa kwenda kuabudu kanisani hapo na
kukutana na wachungaji ambao ndio viongozi wa kanisa.
Lakini pia
kama ukitaka kubatizwa kanisani hapo ni lazima ukubali kuitwa 'Diego' kama jina
lako la katikati ili kumpokea kikwelikweli gwiji huyo kuwa ndio 'mungu' wako wa
soka.
0 comments:
Post a Comment