Ndg Mwanachama wa SIMBA SPORTS CLUB,
TAWI LA SIMBA DUME-TEMBONI
Ile siku inayosubiriwa kwa Hamu yaani 05/08/2015 inawadia na ipo jirani kuanzia sasa, hivyo ni wajibu wako Mwanachama kutekeleza maazimio ya Kikao kilichopita ambacho tuliahidiana Michango ya Sherehe yaani 40,000/= kuwa Jumapili ya tarehe 26/07 ndio mwisho wa kutoa.
Wengi wameshatoa na umebaki wewe tu na unapaswa kuwasilisha mapema kwa viongozi wa tawi au kuja nayo siku ya Jpili 26/07/2015 kwenye kikao kitakachohudhuriwa na wageni maalumu wa ngazi za juu katika nchi hii .
Hupaswi kukosa maana maagizo toka makao makuu ya Simba yataletwa na mgeni maalum kwa niaba ya Rais wa S.S.C.
Kikao kitafanyika pale HOJA MOTEL iliyopo TEMBONI kuanzia saa 9:00 alasiri.
Kumbuka tuko mwishoni kabisa kukamilisha maandilizi ya SHEREHE yetu kubwa ya kufungua tawi la SIMBA DUME-TEMBONI.
"Usikubali kuwa Nyuma, utaachwa".
Taarifa na
Ben Shija
Mwenyekiti wa Tawi...
0 comments:
Post a Comment