Ama kweli leo ni siku ya stori za mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa.
Mwandishi mmoja wa vitabu, Fran Guillen ametoa toleo la kitabu kinachomhusu Costa mwenye miaka 26 kiitwacho “The Art of War,” .
Kuna stori nyingi kwenye kitabu hicho, lakini mbili zinazungumzia namna Costa alivyokataa kujiunga na Liverpool mwaka 2013 na maneno aliyomwambia John Terry siku yake ya kwanza katika uwanja wa mazoezi wa
Cobham.
Kali ya yote, Msimulizi wa kitabu hicho ameliambia gazeti la Mirror kwamba siku moja Costa alimuua bila kukusudia mbwa wake aliyejulikana kwa jina la Yorkshire Terrier.
Kwa mujibu wa stori hiyo, Costa aliwasili na mbwa huyo mjini Madrid, lakini siku moja wakati anarudi nyuma na gari yake kwa lengo la ku-park, kwa bahati mbaya alimkanyaga. Mirror wanaripoti:
"Diego alikuja na mbwa wake Madrid, lakini siku moja wakati ana-park gari hakujua kama mbwa huyo yuko nyuma ya gari, wakati anarudi nyuma akamkanyaga".
"Kitendo hicho kilimfanya Costa awe mnyonge kwa mwezi mmoja. Nilipomuuliza kwanini yuko hivyo aliniambia:
"Siwezi kuamini. Nimemuua mbwa wangu. Alikuja karibu na nyumba yangu kunisalimia na sikumuona, nimemkanyaga".
Kwa sasa Costa ana wasiwasi ya kucheza mechi ya ngao ya Jamii siku ya jumapili dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Wembley baada ya kupata majeruhi tena ya misuli dhidi ya Barcelona katika mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya iliyopigwa wiki nchini Marekani.
Chelsea wataanza msimu wa 2015/2016 kwa kukabiliana na Swansea.
0 comments:
Post a Comment