Msanii wa Comed, Simon Brodkin ambaye alimrushia bunda la dola, Rais wa FIFA, Sepp Blatter amefichua kwamba zile fedha zilikuwa dola 600 na zilikuwa zake,
Wale wanaodhani zilikuwa fedha feki, amesema zilikuwa halali.
Simon amesema kwamba baada ya tukio lile Maafisa wa usalama wa FIFA walimrudishia fedha zote.
Jumatatu ya wiki hii, Brodkin, anayejulikana kwa jina la kicomed la Lee Nelson na Jason Bent alivamia mkutano wa Blatter na waandishi wa habari makao makuu ya FIFA, Zurich, Uswizi na kumrushia bunda la dola.
Alikamatwa na mamlaka za Uswisi, lakini baadaye aliachiwa huru kurejea kwao Uingereza.
Comedian huyo amesema: "Kwa bahati mbaya ishu imekuwa serious. Nina wasiwasi? najua nimepigwa faini na sijui kama naweza kuizungumzia sana".
"Ninachoweza kusema ni kwamba kama ningefungwa jela, ningekuwa mtu wa kwanza kwenda jela kwa tukio lililofayika makao makuu ya FIFA".
Msanii huyo amesema alifanya tukio hilo la utani kwa FIFA kutokana na kashfa ya rushwa inayolizingira shirikisho hilo baada ya uchunguzi wa FBI.
0 comments:
Post a Comment