Manchester United wamefungua mazungumzo na PSG kuhusu usajili wa Angel Di Maria ambaye ameshaonesha nia ya kutimka Old Trafford.
Wiki iliyopita ripoti zilienea Hispania kwamba Di Maria anapenda kurejea katika klabu yake ya Real Madrid, lakini miamba hiyo ilikanusha na sasa PSG ndio sehemu pekee anayoweza kwenda kwani hata Bayern Munich waliokuwa wakihusishwa kumsajili wamechomoa.
Kwa mujibu wa The Star, mazungumzo makubwa ya United na PSG ni kuhusu ada ya uhamisho ya nyota huyo ambaye Man United walimsaini kwa paundi milioni 59 majira ya kiangazi mwaka jana.
Hata hivyo mashetani hao wekundu hawategemei kupata faida katika dili hilo.
0 comments:
Post a Comment