Thursday, July 23, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Heegan FC imeaga rasmi mashindano ya Kombe la Kagame mwaka huu baada ya leo alasiri kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Al Shandy katika mechi yao ya mwisho ya Kundi B iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Al Shandy walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Eid Mugadam dakika ya sita baada ya kiungo mshambuliaji huyo kuwapiga chenga ndani ya boksi mabeki wa Heegan FC kisha kupiga shuti kali la mguu wa kulia ndani ya boksi lililompiga kipa Mohamed Subairu wa timu hiyo ya Somalia.
Goli la pili la timu hiyo ya Sudan lilifungwa na winga Elsadig Hassan kwa mkwaju wa penati ulioamuliwa na refa Ssali Mashood kutoka Uganda baada ya beki wa kati wa Heegan, Harry Gentle kumkwatua mshambuliaji Galal Alpeen ndani ya boksi dakika mbili kabla ya nusu saa ya mchezo.
Hassah Farid, Nahodha wa Heegan FC, aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 70 akifumua shuti kali la mguu wa kulia nje kidogo mwa boksi lililompoita kipa Faoaz Jamal.
Hata hivyo, dakika moja baadaye Mugadam alirudi tena nyavuni akiifungia goli la tatu na la ushindi Al Shandy na kuiaga rasmi Heegan FC mashindanoni.
Dakika tatu baada ya bao hilo kufungwa, yaani dakika ya 84, Nahodha Farid aliifungia Heegan FC bao la pili akifumua shuti kali la mguu wa kulia akiwa ndani ya boksi na kumwacha kipa Jamal akilala bila mafanikio.
Matokeo hayo yameifanya Heegan FC imalize mkiani mwa Kundi B ikiwa na pointi moja iliyoipata katika suluhu dhidi ya LLB FC ya Burundi kwenye Uwanja wa Karume Jumapili.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Somalia ilifungwa 2-0 dhidi ya APR katika mechi yao ya pili iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jumanne.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video