Oscar Joshua akipiga mahesabu ya kumtoka Donald Ngoma Dombo.
"Nina furaha kujiunga na Yanga,ni miongoni mwa klabu kubwa Afrika ina uongozi bora, mashabiki bora,waalimu bora pia na kikosi bora!hatukutegemea kama tungepata mapokezi kama haya kutoka kwa mashabiki (yeye na Zuttah), tumeshangazwa sana na jinsi mashabiki walivyo wengi na wanavyoipenda timu yao.Najua kuchezea klabu kubwa kama hii kuna presha kubwa sana lakini naamini nitaishinda hiyo presha na kufanya kile mashabiki wanachotaraji kutoka kwangu,siwezi ahidi chochote zaidi ya kusema kazi yangu uwanjani ndio itatoa majibu", alisema Mzimbabwe Donald Ngoma Dombo anayeondoka leo kurudi kwao kwa ajili ya kujiandaa rasmi ili kuitumikia Yanga ambapo atarudi jumapili na siku ya jumatatu ataanza mazoezi.
Joseph Tetteh Zuttah yeye hatorudi kwani tayari alishajiandaa.
0 comments:
Post a Comment