Didier Drogba anaamini kuwa Rio Ferdinand, Nemanja Vidic Carles Puyol ndio mabeki bora kabisa ambao amewahi kukutana nao katika kipindi chote cha maisha yake ya soka.
Drogba, 37, alifunga goli la ushindi kwenye fainali ya kombe la FA mwaka 2007 dhidi ya Manchester na pia aliwahi kutolewa nje katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2008 dhidi ya Man United baada ya kumpiga kofi Nemanja Vidic, mchezo ambao Chelsea walipoteza kwa matuta.
Drogba pia amewahi kukumbana na Puyol mara nane katika kipindi chake cha soka na amefanikiwa kufunga mara tatu mbele ya Mlinzi huyo, wakati walipokuwa wakikutana katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya.
Akifanya mahojiano na Rio Ferdinand katika moja ya vipindi vya BT Sport, Drogba aliulizwa na Ferdinand kutaja mabeki wagumu ambao amewahi kukutana nao.
“Siku zote nimekuwa nikisema ni wewe na Vidic,” Drogba alijibu. “Ninaweza kusema kuwa wakati nilipokuwa nikifunga dhidi ya Manchester United nilikuwa nafurahi sana kwa sababu sikufunga mara nyingi sana dhidi yao.
“Hivyo kwangu mimi, kufunga dhidi yenu ninyi, ilimaanisha kuwa nilikuwa kwenye kiwango bora siku hiyo!
“Hivyo,ninyi wawili pamoja na Carles Puyol ndio noma. sababu, mfano Puyol ni beki mzuri sana, ni mgumu kupitika na ni mwepesi, lakini ni mtu poa sana”. Alimalizia
0 comments:
Post a Comment