UONGOZI wa
Yanga umetoa baraka kwa mshambuliaji wake, Kpah Sherman ambaye anatarajia
kuondoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afya katika moja
ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo kabla ya kukamilisha usajili.
Sherman ameingia sokoni kutokana na uwezo wake kutolifurahisha benchi la
ufundi la Yanga huku kukiwa na ushindani mkali wa namba ambapo washambuliaji
wengine waliopo kikosini hapo ni Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Malimi Busungu.
Katibu Mkuu
wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amesema kuwa, wapo katika mazungumzo ya mwisho na
timu hiyo inayomhitaji Sherman.
“Dili lipo
katika hatua za mwisho na pindi litakapokuwa sawa ataondoka nchini kwa ajili ya
kufanya vipimo na endapo atafuzu basi atajiunga na timu hiyo ambayo siwezi
kukutajia jina kwa sasa.
“Hatupendi
aende huko halafu akapate tabu ila tunatata akacheze soka, ndiyo maana
hatukutaka aende kwa ajili majaribio kwani hiyo siyo hadhi yake,” alisema
Tiboroha.
Inaelezwa kwamba, Sherman ataondoka keshokutwa Jumapili au Jumatatu kujiunga na timu ya
Mpumalanga Black Aces.
0 comments:
Post a Comment