Na Ramadhani ngoda.
Licha ya kukanusha
taarifa za Paul Pogba kuwa njiani kuelekea Fc Barcelona kutokana na mzungumzo
ya wiki iliopita, raisi wa Juventus Turin, Andrea Agnelli amekiri kuwa kiungo
huyo muda wowte ataondoka klabuni hapo katika majira haya ya joto.
Matajiri wa jiji la
Manchester klabu ya Manchesetr City wanaaminika kuwa wako tayari kutoa kiasi
kinachohitajika na vibibi vizee hivyo vya jiji la Turin cha pauni milioni 70,
lakini kiungo huyo anaweza kuwa na nafasi kubwa Zaidi ya kujiunga na mabingwa
wa Hispania na Ulaya, Fc Barcelona.
Mabingwa wa Ufaransa PSG
wakiwa miongoni mwa timu zinazowania dole gumba la kiungo huyo, moja ya watu
wanaowania nafasi ya uraisi katika klabu ya Fc Barcelona Juan Laporta,
amemuweka Pogba kama sehemu ya ahadi katika kampeni zake mwaka huu.
Kauli ya kuonesha
kukata tamaa kwa Juve juu ya Pogba iliyotokewa na raisi Agnelli imekuja ikiwa
ni wiki moja tu tangu akanushe vikali fununu za Mfaransa huyo kuelekea Camp Nou
ambapo Barca walikuwa tayari kumuacha kwa msimu mmoja Juventus kutokana na
adhabu yao ya kutosajili.
“Hakuna kilichopo kwa
100% katika soka. Unaweza kusema mchezaji hauzwi kuanzia tarehe 1 Septemba
(dirisha litakuwa limefungwa),” alisema Agnelli katika mkutano na waandishi wa
habari.
“Miaka kadhaa
iliyopita, tulisema Christian Vieri hauzwi, lakini alielekea Atletico Madrid
siku chache tu zilizofuata,” alisisitiza raisi huyo.
Pogba (22)
aliyebakisha miaka mine kwenye kanfarasi yake Juventus, ameshaiwakilisha timu
yake ya taifa katika ngazi zote na ameshashinda ligi kuu Italia mara 3, na
kuisadia timu yake kufika fainali na ligi ya mabingwa msimu uliyomalizika na
kushuhudia Barcelona wakiibuka machampioni.
0 comments:
Post a Comment