Na Ramadhani Ngoda.
Licha ya uvumi
uliotanda kuwa anaweza kuondoka Santiago Bernabeu, mlinzi wa klabu hiyo
Mhispania Dani Carvajal amejitia kitanzi kwa kuongeza mkataba wake utakaomuweka
Bernabeu hadi 2020.
Awali tetesi
zilieleza kuwa mlinzi huyo wa kulia angeweza kumpisha Mbrazil Danilo Luiz Da
Silva aliyesajiliwa akitokea Fc Porto ya nchini Ureno na kuonekana kuwa katika
malengo ya kocha mpya Rafa Benitez.
Mlinzi huyo wa
kimataifa wa Hispania ambaye alibakisha miaka 4 kwenye mkataba wake, ameamua
kupigana kupata namba ndani ya mabingwa hao wa Ulaya wa mwaka 2014 licha ya kuwa na
upinzani kutoka kwa Danilo.
Carvajal (23)
alitokea kwenye timu ya vijana ya Real kabla ya kutimkia nchini Ujerumani kunako
klabu ya Bayer04 Leverkusen mwaka 2012.
Madrid walifanikiwa
kumrudisha beki huyo msimu uliofuata kutokana na mkataba wake kuwa na kipengele
ambacho kingeweza kumrejesha Bernabeu wakilazimika kulipa kiasi cha Yuro
milioni 6.5 tu na baada ya kukaa Bayarena kwa msimu mmoja pekee.
Tangu kurejea kwake
amekuwa akipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya
mji mkuu wa Hispania na kuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda ligi ya mabingwa na
Copa Del Rey msimu wa 2013/14 chini ya kocha ‘aliyetalikiwa’ Carlo Anceloti.
0 comments:
Post a Comment