Mabingwa wa soka nchini UJERUMANI, BAYERN MUNICH leo wamekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa CHILE na JUVENTUS, ARTURO VIDAL na kumsainisha mkataba wa miaka minne.
Vidal ambaye amerithi nafasi ya BASTIAN SCHWEINSTEIGER aliyetimkia MANCHESTER UNITED majira haya ya kiangazi ametua kwa miamba hiyo ya Bundesliga kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 28.
Muda mfupi baada ya kumwaga wino, VIDAL amesema kwamba anafurahia kujiunga na Bayern ingawa amekiri kukabiliwa na changamoto ya kufanya vyema.
VIDAL mwenye miaka 28 amesema lengo lake kubwa ni kushinda makombe makubwa kama ligi ya mabingwa Ulaya, hivyo anaamini nafasi hiyo ipo Bayern.

0 comments:
Post a Comment