Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KUMBE kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi ameuzwa katika klabu ya Sonderjsyke ya Denmark, imefahamika.
Okwi; aliyeibeba Simba kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu uliopita, anatarajiwa kuiunga na klabu hiyo muda wowote akitokea Mauritius alikokwenda kwa ajili ya fungate baada ya kufunga ndoa hivi karibuni.
Zacharia Hanspope, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, ametoa taarifa muda mfupi uliopita wakati akihojiwa na moja ya redio za jijini hapa na kuweka wazi kwamba Okwi ameuzwa katika klabu hiyo na si kwamba anakwenda kwa mkopo kama ilivyodaiwa na Rais wa Simba, Evans Aveva mapema leo.
"Okwi tumemuuza Denmark kwa dau ambalo hatuwezi kuliweka wazi kwa sababu mnaweza kutuvamia," amesema Hanspope na kueleza zaidi kuwa Okwi atatoka Mauritius na kuunganisha mojan kwa moja kwenda kujiunga na klabu hiyo.
Okwi aliwahi pia kuzitumikia Etoile du Sahel ya Tunisia, Yanga na SC Villa ya kwao Uganda iliyomkuza.
0 comments:
Post a Comment